Deuteronomy 26:1-6

Malimbuko Na Zaka

1Mtakapokuwa mmeingia nchi ile ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa kama urithi na mtakapokuwa mmeimiliki na kukaa ndani yake, 2 achukueni baadhi ya mavuno ya kwanza ya yale yote mtakayozalisha kutoka udongo wa nchi ambayo Bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa na mweke kwenye kapu. Kisha uende mahali ambapo Bwana Mwenyezi Mungu wako atapachagua kuwa makao kwa ajili ya Jina lake 3na umwambie kuhani atakayekuwepo kwa wakati huo, “Ninatangaza leo kwa Bwana Mwenyezi Mungu wako kwamba nimekuja katika nchi ambayo Bwana aliwaapia baba zetu kwamba atatupa.” 4Kuhani atapokea lile kapu mikononi mwako na kuliweka chini mbele ya madhabahu ya Bwana Mwenyezi Mungu wako. 5 bKisha utatangaza mbele za Bwana Mwenyezi Mungu wako: “Baba yangu alikuwa Mwaramu aliyekuwa anatangatanga, akaenda Misri pamoja na watu wachache, akaishi huko hadi akawa taifa kubwa, lenye nguvu na watu wengi. 6 cLakini Wamisri walituonea na kututaabisha, wakitufanyisha kazi ngumu.
Copyright information for SwhKC